Ezekieli3
1Naye akaniambia, “Mwanadamu, kula kilichoko mbele yako, kula kitabu hiki, kisha uende ukaseme na nyumba ya Israeli.”2Hivyo, nikafungua kinywa changu, naye akanipa kile kitabu nikile.3Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, kula kitabu hiki ninachokupa, ujaze tumbo lako.” Kwa hiyo nikaula, nao ulikuwa mtamu kama asali kinywani mwangu.4Kisha akaniambia, “Mwanadamu, sasa nenda katika nyumba ya Israeli ukawanenee maneno yangu.5Hukutumwa kwa taifa lenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli.6Sikukutuma kwa mataifa mengi yenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu ambao maneno yao hutayaelewa. Hakika ningekutuma kwa watu hao, wangekusikiliza.7Lakini nyumba ya Israeli haitakusikiliza, kwa kuwa hawako radhi kunisikiliza mimi, kwa kuwa nyumba yote ya Israeli ni wenye paji gumu na mioyo ya ukaidi.8Tazama, nimefanya uso wako mgumu dhidi ya nyuso zao, na paji la uso wako gumu dhidi ya paji za nyuso zao.9Kama vile almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyolifanya paji la uso wako. Usiwaogope wala usiwahofu, ijapokuwa ni nyumba ya uasi.”10Naye akaniambia, “Mwanadamu, sikiliza kwa makini na uyatie moyoni mwako maneno yote nitakayosema nawe.11Kisha nenda kwa watu wa taifa lako walio uhamishoni, ukaseme nao. Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi’; iwe watasikiliza au hawatasikiliza.”12Ndipo Roho wa Mungu akaniinua juu, nami nikasikia sauti kubwa ya ngurumo nyuma yangu ikisema, “Utukufu wa Mwenyezi Mungu na utukuzwe katika makao yake!”13Ilikuwa ni sauti ya mabawa ya wale viumbe hai yakigusana moja kwa lingine, na sauti ya magurudumu kando yao, sauti kubwa ya ngurumo.14Kisha Roho wa Mungu akaniinua juu na kunipeleka mbali. Nikaenda nikiwa na uchungu na hasira moyoni mwangu, nao mkono wenye nguvu wa Mwenyezi Mungu ukiwa juu yangu.15Nikafika kwa wale watu waliokuwa uhamishoni huko Tel-Abibu karibu na Mto Kebari. Nikakaa miongoni mwao kwa muda wa siku saba, nikiwa nimejawa na mshangao.