Kutoka25swh_onmm
Sadaka kwa ajili ya maskani ya Mungu
1Mwenyezi Mungu akamwambia Musa,2“Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea sadaka kwa niaba yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa.3“Hizi ndizo sadaka utakazozipokea kutoka kwao:“dhahabu, fedha na shaba;4nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu, pamoja na kitani safi; singa za mbuzi;5ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo; mbao za mshita;6mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezo kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri;7na vito vya shohamu na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kizibau na kile kifuko cha kifuani.8“Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao.9Tengeneza Maskanihii na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonesha.