Mhubiri12swh_onmm
1Mkumbuke Muumba wakosiku za ujana wako,kabla hazijaja siku za taabu,wala haijakaribia miaka utakaposema,“Mimi sifurahii hiyo”:2kabla jua na nuru,nao mwezi na nyota havijatiwa giza,kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;3siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka,nao watu wenye nguvu watakapojiinamisha,wakati wasagao watakapokoma kwa sababu ya uchache,nao wachunguliao madirishani kutiwa giza;4wakati milango ya kuingia barabarani itakapofungwana sauti ya kusaga kufifia;wakati watu wataamshwa kwa sauti ya ndege,lakini nyimbo zao zote zikififia;5wakati watu watakapoogopa kilichoinuka juuna hatari zitakazokuwepo barabarani;wakati mlozi utakapochanua mauana panzi kujikokotanawe usiwe na shauku ya kitu chochote.Ndipo mwanadamu aiendea nyumba yake ya milelenao waombolezaji wakizunguka barabarani.6Mkumbuke Muumba wako: kabla haijakatika kamba ya fedha,au bakuli la dhahabu halijavunjika;kabla mtungi kuvunjika kwenye chemchemi,au gurudumu kuvunjika kisimani,7nayo mavumbi kurudi ardhini yalikotoka,na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.8Mhubiri asema, “Ubatili! Ubatili!Kila kitu ni ubatili!”