1Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema:“Piga vichwa vya nguzoili vizingiti vitikisike.Viangushe juu ya vichwa vya watu wote;na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga.Hakuna yeyote atakayekimbia,hakuna atakayetoroka.2Wajapojichimbia chini hadi kwenye vina vya Kuzimu ,kutoka huko mkono wangu utawatoa.Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu,kutoka huko nitawashusha.3Wajapojificha juu ya kilele cha Karmeli,huko nitawawinda na kuwakamata.Wajapojificha uso wangukatika vilindi vya bahari,huko nako nitaamuru joka kuwauma.4Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao,huko nako nitaamuru upanga uwaue.Nitawakazia macho yangu kwa mabayawala si kwa mazuri.”5Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni,yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka,na wote wanaoishi ndani yake wakaomboleza:nayo nchi yote huinuka kama Mto Naili,kisha hushuka kama mto wa Misri;6yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbinguna kuisimika misingi yake juu ya dunia,yeye aitaye maji ya baharina kuyamwaga juu ya nchi:Mwenyezi Mungu ndilo jina lake.7“Je, Waisraeli,ninyi si sawa kwangu kama Wakushi?”asema Mwenyezi Mungu.“Je, sikuleta Israeli kutoka Misri,Wafilisti kutoka Kaftori ,na Washamu kutoka Kiri?8“Hakika macho ya Bwana Mungu Mwenyeziyako juu ya ufalme wenye dhambi.Nami nitauangamizakutoka uso wa dunia:hata hivyo sitaiangamiza kabisanyumba ya Yakobo,”asema Mwenyezi Mungu.9“Kwa kuwa nitatoa amri,na nitaipepeta nyumba ya Israelimiongoni mwa mataifa yote,kama vile nafaka ipepetwavyo katika ungo,na hakuna hata punje moja itakayoanguka chini.10Watenda dhambi wote miongoni mwa watu wanguwatauawa kwa upanga,wale wote wasemao,‘Maafa hayatatupata wala kutukuta.’
Kurejeshwa kwa Israeli
11“Katika siku ile“Nitalisimamisha hema la Daudi lililoanguka.Nitakarabati mahali palipobomokana kujenga upya magofu yake,na kuijenga kama ilivyokuwa awali,12ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu,na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,”asema Mwenyezi Mungu ambaye atafanya mambo haya.13“Siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu,“wakati mvunaji atatanguliwa na mkulima,naye mpanzi atatanguliwa na yeye akamuaye zabibu.Divai mpya itadondoka kutoka milimani,na kutiririka kutoka vilima vyote.14Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa;wataijenga tena miji iliyoachwa magofu,nao wataishi ndani yake.Watapanda mizabibu na kunywa divai yake;watalima bustani na kula matunda yake.15Nitaipanda Israeli katika nchi yao wenyewe,hawatang’olewa tenakutoka nchi niliyowapa,”asema Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.