Amosi2swh_onmm

1Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:“Kwa dhambi tatu za Moabu,hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu,ikawa kama chokaa.2Nitatuma moto juu ya Moabuambao utateketeza ngome za Keriothi.Moabu ataanguka kwa ghasia kubwakatikati ya kelele za vita, na sauti ya tarumbeta.3Nitamwangamiza mtawala wakena kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,”asema Mwenyezi Mungu.4Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:“Kwa dhambi tatu za Yuda,hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.Kwa sababu wameikataa Torati ya Mwenyezi Munguna hawakuzishika amri zake,kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo,miungu ambayo babu zao waliifuata.5Nitatuma moto juu ya Yudaambao utateketeza ngome za Yerusalemu.”

Hukumu kwa Israeli

6Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:“Kwa dhambi tatu za Israeli,hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.Wanawauza wenye haki kwa fedha,na maskini kwa jozi ya viatu.7Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini,kama vile juu ya mavumbi ya nchi,na kukataa haki kwa waliodhulumiwa.Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja,kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu.8Watu hulala kando ya kila madhabahujuu ya nguo zilizowekwa rehani.Katika nyumba ya mungu wao hunywa mvinyoulionunuliwa kwa fedha walizotozwa watu.
9“Nilimwangamiza Mwamori mbele yao,ingawa alikuwa mrefu kama mierezi,na mwenye nguvu kama mialoni.Niliyaangamiza matunda yake juuna mizizi yake chini.
10“Niliwapandisha toka Misri,na nikawaongoza miaka arobaini jangwaniniwape nchi ya Waamori.
11“Pia niliinua manabii kutoka miongoni mwa wana wenuna Wanadhiri kutoka miongoni mwa vijana wenu.Je, hii si kweli, enyi watu wa Israeli?”asema Mwenyezi Mungu.12“Lakini mliwafanya Wanadhiri kunywa mvinyona kuwaamuru manabii wasitoe unabii.
13“Sasa basi, nitawapondakama gari linavyoponda likiwa limejazwa nafaka.14Mkimbiaji hodari hatanusurika,wenye nguvu wataishiwa nguvu zao,na shujaa hataweza kuokoa maisha yake.15Mpiga upinde atakimbia,askari wapiga mbio hawataweza kutoroka,na mpanda farasi hataokoa maisha yake.16Hata askari walio mashujaa sanasiku hiyo watakimbia uchi,”asema Mwenyezi Mungu.