Amosi1swh_onmm
1Maneno ya Amosi, mmoja wa wachungaji wa Tekoa: yale aliyoyaona kuhusu Israeli miaka miwili kabla ya tetemeko la ardhi, wakati Uzia alikuwa mfalme wa Yuda, na Yeroboamu mwana wa Yehoashi alikuwa mfalme wa Israeli.2Alisema:“Mwenyezi Mungu ananguruma toka Sayuni,pia ananguruma kutoka Yerusalemu;malisho ya wachungaji yanakauka,kilele cha Karmeli kinanyauka.”