2 Yohana1
Salamu
1Mzee.Kwa mama mteule na watoto wake, ninaowapenda katika kweli; wala si mimi tu, bali na wale wote wanaoijua kweli;2kwa sababu ya ile kweli inayokaa ndani yetu, na ambayo itaendelea kukaa nasi milele.3Neema, rehema na amani zinazotoka kwa Mungu Baba Mwenyezi na kwa Isa Al-Masihi, Mwanawe Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.