2 Mambo Ya Nyakati29swh_onmm
Hezekia mfalme wa Yuda
1Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria.2Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu kama Daudi baba yake alivyofanya.3Katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa kwanza wa utawala wake, alifungua milango ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, na kuikarabati.4Akawaingiza makuhani na Walawi ndani na kuwakutanisha katika uwanja upande wa mashariki5na kusema: “Nisikilizeni mimi, enyi Walawi! Jitakaseni nafsi zenu sasa, mkalitakase Hekalu la Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu. Ondoeni uchafu wote kutoka mahali patakatifu.6Baba zetu hawakuwa waaminifu, walifanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, na wakamwacha yeye. Wakageuza nyuso zao mbali na Maskani ya Mwenyezi Mungu wakamgeuzia visogo vyao.7Pia walifunga milango ya ukumbi wa Hekalu na kuzima taa zake. Hawakufukiza uvumba wala kutoa sadaka yoyote ya kuteketezwa katika mahali patakatifu kwa Mungu wa Israeli.8Kwa hiyo, hasira ya Mwenyezi Mungu ikashuka juu ya Yuda na Yerusalemu, naye akawa amewafanya kitu cha kutisha, cha kushangaza na kitu cha kufanyia mzaha kama mnavyoona kwa macho yenu wenyewe.9Hii ndiyo sababu baba zetu wameanguka kwa upanga na ndiyo sababu wana wetu wa kiume na wa kike, na pia wake zetu wamekuwa mateka.10Sasa ninadhamiria moyoni mwangu kufanya agano na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ili hasira yake kali igeuziwe mbali nasi.11Wanangu, basi msipuuze jambo hili sasa, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewachagua ninyi msimame mbele zake na kumtumikia, mkawe watumishi wake na mkamfukizie uvumba.”12Ndipo Walawi wafuatao wakaanza kazi:Kutoka kwa Wakohathi, Mahathi mwana wa Amasai na Yoeli mwana wa Azaria; kutoka kwa Wamerari, Kishi mwana wa Abdi na Azaria mwana wa Yahaleleli; kutoka kwa Wagershoni, Yoa mwana wa Zima na Edeni mwana wa Yoa;13kutoka kwa wana wa Elisafani, Shimri na Yeieli; kutoka kwa wana wa Asafu, Zekaria na Matania;14kutoka kwa wana wa Hemani, Yehieli na Shimei; kutoka kwa wana wa Yeduthuni, Shemaya na Uzieli.15Walipomaliza kuwakusanya ndugu zao na kujiweka wakfu, wakaingia ndani ili kutakasa Hekalu la Mwenyezi Mungu, kama vile mfalme alivyokuwa ameagiza, kwa kufuata neno la Mwenyezi Mungu.16Makuhani wakaingia patakatifu pa Hekalu la Mwenyezi Mungu ili kupatakasa. Wakatoa nje penye ua wa Hekalu la Mungu kila kitu kichafu walichokikuta kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu. Walawi wakavichukua na kuvipeleka nje katika Bonde la Kidroni.17Walianza kazi ya utakaso siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza na kufikia siku ya nane ya mwezi huo wakawa wamefikia kwenye ukumbi wa Mwenyezi Mungu. Kwa siku zingine nane wakalitakasa Hekalu la Mwenyezi Mungu lenyewe, wakakamilisha katika siku ya kumi na sita ya mwezi huo wa kwanza.18Kisha wakaingia ndani kwa Mfalme Hezekia kutoa habari na kusema: “Tumelitakasa Hekalu la Mwenyezi Mungu lote, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa pamoja na vyombo vyake vyote, meza ya kupanga mikate iliyowekwa wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote.19Tumeviandaa na kuvitakasa vyombo vyote ambavyo Mfalme Ahazi, kwa kukosa uaminifu kwake, aliviondoa alipokuwa mfalme. Sasa viko mbele ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu.”