1 Petro1
Salamu
1Petro, mtume wa Isa Al-Masihi.Kwa wateule wa Mungu, wageni katika ulimwengu, waliotawanyika kote katika Ponto, Galatia, Kapadokia, jimbo la Asia, na Bithinia.2Ni ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba Mwenyezi kulingana na alivyotangulia kuwajua, kupitia kwa kazi ya utakaso wa Roho wa Mungu, katika utiifu kwa Isa Al-Masihi na kunyunyiziwa damu yake.
Neema na amani ziwe kwenu kwa wingi.