1 Wafalme4swh_onmm
Maafisa na watawala wa Sulemani
1Basi Mfalme Sulemani akatawala Israeli yote.2Hawa walikuwa maafisa wake wakuu:Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki;3Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani;4Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi; Sadoki na Abiathari: makuhani;5Azaria mwana wa Nathani: kiongozi wa maafisa wa wilaya; Zabudi mwana wa Nathani: kuhani na mshauri binafsi wa mfalme;6Ahishari: msimamizi wa jumba la kifalme; Adoniramu mwana wa Abda: msimamizi wa kazi za kulazimisha.7Pia Sulemani alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioshughulikia mahitaji ya mfalme na ya watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka.8Majina yao ni haya:
Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu;9Ben-Dekari: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Beth-Hanani;10Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake);11Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Sulemani);12Baana mwana wa Ahiludi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Sarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu;13Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makazi ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa yake, kadhalika wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini iliyozungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba);14Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu;15Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Sulemani);16Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi;17Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari;18Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini;19Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa mtawala pekee katika eneo hilo.