1 Mambo Ya Nyakati5swh_onmm
Wana wa Reubeni
1Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa.2Na ingawa Yuda alikuwa na nguvu zaidi ya ndugu zake wote, na mtawala alitoka kwake, haki za mzaliwa wa kwanza zilikuwa za Yusufu.)3Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli walikuwa:Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.4Wazao wa Yoeli walikuwa: Shemaya mwanawe, Gogu mwanawe; Shimei mwanawe,5Mika mwanawe, Reaya mwanawe, Baali mwanawe,6na Beera mwanawe, ambaye Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alimchukua kwenda uhamishoni. Beera alikuwa kiongozi wa Wareubeni.7Jamaa zao kulingana na koo zao, walioorodheshwa kwa koo zao kama ifuatavyo: Yeieli aliyekuwa mkuu wao, Zekaria,8Bela mwana wa Azazi, mwana wa Shema, mwana wa Yoeli.
Hao waliishi katika eneo lililoanzia Aroeri hadi Nebo na Baal-Meoni.9Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea hadi kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi.10Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao. Kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki mwa Gileadi.