1 Mambo Ya Nyakati3swh_onmm
Wana wa Daudi
1Hawa walikuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni:Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli; wa pili, Danieli ambaye mama yake aliitwa Abigaili wa Karmeli;2wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake aliitwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, ambaye mama yake aliitwa Hagithi;3wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake aliitwa Abitali; wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.4Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita.
Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na tatu,5nao hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu:
mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia wana wanne: Shamua, Shobabu, Nathani na Sulemani.6Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti,7Noga, Nefegi, Yafia,8Elishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa.9Hawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao.